Familia moja kutoka kijiji cha Mukulusu eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega imelazimika kukesha nje kwa kijibaridi baada ya moto kuteketeza mali ya maelefu ya pesa ndani ya nyumba zao tatu kwa njia tatanishi.

Jamii hiyo ikiongozwa na mzee Peter Liyayi na Regina Kakai Jumba, inasema chanzo cha moto huo kimesalia kitendawili kwani ulilipuka kwa njia ya kutatanisha na kuchoma vyomba vya nyumba vikiwemo viti, meza, televisheni kati ya vyombo Vinginezo wakitoa wito kwa wahubiri kuingilia kati na kuwasaidia kwa maombi.

Wanadai hii ni mara ya tatu imepelekea hata wanao kukosa masomo kwani wanaenda shuleni wakiwa darasani wao uandamwa na moto huo hadi darasani, wakidai huenda wamesukumiwa majini.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE