Wakazi wa kijiji cha Kamwega eneo la Shinyalu mpakani mwa kaunti za Kakamega na Nandi Wameshangazwa baada ya mwanamme wa miaka 52 kufukua kaburi la mwanawe kwa madai kuwa alikuwa amezikwa  vibaya na pia mkewe amekuwa akishiriki mapenzi na mwanawe wa kiume wakapata mwendazake..

Wanakijiji wakiongozwa na Florence Sambaya na Charles Musee, wanasema mshukiwa Aggrey Siema alianza kufukua kaburi la mwanawe wa miaka 14 wa kike aliyezikwa jumatano kwa madai kuwa alikuwa amezikwa vibaya akitaka kufukua ili aweze kuzika upya.

Vilevile mshukiwa alidai kuwa mkewe amekuwa akishiriki ngono na mwanawe wa kiume ambaye walifanikiwa kupata mwendazake Lilian Aseya aliyezikwa jumatano akitaka kuufukua mwili huo.

Hata hivyo maafisa wa polisi kutoka kituo cha Kamwega walifika kwa haraka na kumtia mbaroni hadi kituo cha polisi na kisha kumwachilia huru.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE