Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Ambetsa Oparanya sasa anashinikiza kubuniwa kwa sheria ambayo itawasaidia viongozi wa kisiasa ambao walichaguliwa kulipwa marupurupu ya uzeeni ili kuwaondolea viongozi hao masaibu ambayo huwakumba baada ya kutemwa nje na wapiga kura

Akizungumza baada ya kukutana na mawaziri na wakilishi wadi wa kaunti hii, Oparanya ameskitikia hali ngumu ambayo baadhi ya wakilishi wadi ambao hawakurejea kwa awali pili jinsi wanavyosumbuka, akidokeza kuwa swala hilo baraza la magavana nchini liliwasilisha kwa mkuu wa sheria ambaye aliyataka mabunge ya kaunti za humu nchini kubuni sheria hiyo

Spika wa bunge la Kakamega Morris Buluma akiongea kwenye mkutano huo,amesema wao kwenye muungano wa mabunge ya kaunti walishughulikia mswada  huo na kuwasilisha kwa baraza la magavana kuufanyia marekebisho akisitiza kuwa iwapo utapitishwa utawafaa sana siku za usoni

Ni swala ambalo mwakilishi wadi ya Khalaba Boniface Osanga amelisikitikia akisema kuwa mswada huo umekawia kupitishwa kuwa sheria jinsi ilivyo na wabunge na kuwataka wakilishi wadi kuwepesi  kupitisha mswada pindi tu itakapowasilishwa bungeni 

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE