Kuna hofu ya mkurupuko wa magonjwa kwenye soko la Makunga wilayani
Navakholo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa
Kulingana na wafanyibiashara sokoni humo hii ni kutokana na mrundiko wa
taka ambazo zimekaa kwa muda wa miaka 2 sasa
Licha ya soko hilo kugeuka makaazi ya wanyama hatari na hata nyuki
wafanyibiashara hao walohamia maeneo ya nje ya soko sasa wanadai uvundo
mkali kuwafuruaha toka sokoni humo
Kando na hayo wafanyibiashara hao wanalalamikia utovu wa usalama sokoni
humo wakiwanyoshea kidole Cha lawama polisi kwenye kituo cha Makunga kwa
kutowapa usalama wa kutosha
Soko Hilo la Makunga limesalia bila kujengwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa
licha ya ujio wa ugatuzi huku tetesi zikisema kwamba Ni kutokana na
mzozo wa umiliki wa soko hilo baina ya manispaa ya kaunti ndongo ya
Navakholo na Ile ya Mumias Mashariki
Story by James Nadwa