Baadhi ya viongizi wamekuwa na kongamano kuhusiana na mchakato wa BBI ambayo itawafaidi mwananchi hasa katika bonde la ufa.

Akihutubia waandishi wa habari mjini Eldoret gavana wa kaunti ya Elgeyo Marakwet na akiwa mwenyekiti wa BBI katika bonde la ufa Alex Tolgos amewashauri wakazi wa kutika eneo hili kuzingatia suala la BBI kwa kuhamasishwa jinsi itawafaidi hasa kimaendeleo.

Hata hivyo mwenyekiti wa maendeleo ya akina mama kutoka kaunti ya Nandi Sarah Kosgey ameunga mkono suala la mchakato wa BBI kwani wanawake watanufaika na suala la usawa wa kijinsia pale ambapo kiketi cha seneta kitasimamiwa na wanawake wawili ilhali hapo awali kulikuwa na mwakilishi wa akina mama akiwa mmoja.

Kando na hayo,  gavana Tolgos ameongea kuhusiana utovu wa usalama eneo la Kapedo kwa kusema kuwa eneo hilo litanufaika na mchakato wa BBI pale ambapo rasilimali itaweza kuwafikia wananchi na huenda wakabadilisha shughuli zao za kiuchumi bali na kufuga mifugo.

Aidha, ametoa mapendekezo kwa idara ya usalama kuweza kuweka wazi wanaohusika na suala la Kapedo ama kuwaua kwani wameathiri shughuli zao.

Story by Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE