Jamii ya batsotso iliyoko katika eneo bunge la Navakholo imeanza mchakoto wa kujiondoa kutoka katika eneo bunge hilo na kutaka kujiunga na wenzake walioko eneo bunge la Lurambi wakidai kuwa wametelekezwa chini ya uongozi wa mheshimiwa Wangwe.

Jamii hiyo ikiongozwa na aliyekuwa diwani wa Butsotso Magharibi Joseph Lumbasi imesema kuwa kushikanishwa kwao na jamii ya Banyala ilichochewa kisiasa ili kuongeza idadi ya jamii hiyo kupata eneo bunge kutoka kwa ile iliyokuwa Lurambi ya zamani na sasa wakati umefika wao kurudi nyumbani na kuendeleza desturi za kama Watsotso katika eneo la Lurambi pamoja

Ni kauli ambayo imeshabikiwa na wazee eneo hilo wakisema kuwa mila na desturi za jamii hizi mbili haziendanishi kivyovyote na wao kuendelea kuwa eneo bunge hilo wanajipata kukosa mengi na uhuru wao wa kutangamana kama jamii ya Batsotso kama wanavyoelezea wazee Amaraka Kotia, Haningiton Imbukwa, Isaac Khamulatia na Daniel Chimoti.


Wakiongea baada ya kukuwa na kikao cha kujadili mchakato huo katika kanisa la Episcopal Esumeyia wanajamii hao wamesema kuwa wamekuwa wakitumia vibaya kujaza idadi ya wengine ambao kwa sasa hawaoni matunda yeyote huku huduma ukiwa mbaya kuwa kukosa uwakilishi bora jinsi wanavyohoji Moses Akhonya, Joseph Opanda na kiongozi wa watu walio na changamoto za maumbile Richard Kwendo.

Kilio cha jamii hii kimekuwa kikiendelea chini kwa chini wakilalamikia kutengwa kwa miradi mbalimbali na sasa wanaitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutathimini upya mipaka hiyo ya Lurambi na Navakholo ili washikamane na eneio bunge la Lurambi waliko wenzao kulingana na kiongozi wa vijana eneo hilo Benard Omurunga.

Story By Kefa Linda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE