Wanabiashara katika soko la Shibuli eneo bunge la Lurambi wametaka idara inayohusika na masoko katika serikali ya kaunti ya Kakamega kufanya haraka na kuweka usimamizi kwenye soko hilo kusaidia utendakazi wa karibu.

Wakiongea kwenye hafla ya kuutazama mwili wa mmoja wao aliyeaga Ernest Opoti, wanabiashara hao Sachiel Chibole, Shadrack Omurunga na Beatrice Asakhulu wote kwa mtawalia wamesema tangu mwenyekiti wao Joel Kadi kuaga dunia miaka mitatu iliyopita uongozi kwenye soko hilo unayumbayumba.

Wametaja hali mbaya ya mazingira ya kazi ambapo soko hilo halina vyoo vya kujisaidia na uchafu ambao wanahisi huenda wakapatwa na mkurupuko wa magonjwa yanayoletwa na uchafu huku wakilaumu serikali ya kaunti ya Kakamega kwa utepetevu huo, na kusisitiza kuwa huduma bora ni haki yao kwani wao kama wengine hutozwa ushuru.

Sasa wafanyibiashara hao wakiongozwa na Barnabas Machoni wametishia kuandaa maandamano hadi kwa afisi za Gavana Oparanya ili kuwasilisha malalamiko yao iwapo afisi husika haitaajibikia swala hilo la kuhakikisha kuna uongozi katika soko hilo lililoko kwenye barabara kuu ya kakamega mumias na pia kushughulikia hali ya usafi.

Story by Kefa Linda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE