Askofu wa kanisa la kiangilikana Kanda ya Mumias Joseph Wandera ametaja
ufisadi kama chanzo cha kudorora kwa uchumi eneo la Magharibi
Kwenye mahojiano ya kipekee na idhaa hii Wandera amehusisha ufisadi na
kuanguka kwa baadhi ya viwanda kikiwemo kile Cha Mumias
Amesema kuwa sharti vitengo vya serikali vilivyotwikwa jukumu la
kukabili ufisadi vipewe nguvu zaidi kuwafunga wafisadi na hata faini ya
juu kwa wahusika ili liwe funzo kwa wengine
Aidha ameitaka serikali kujumuisha somo la ufisadi kwenye mtaala kama
njia mojawapo ya kujenga vizazi vijavyo visivyo na ufisadi
Kando na uhamasisho askofu huyo anasema kuwa wanahusisha mabaraza,
shule na hata vyombo vya habari kutoa mafunzo dhidi ya ufisadi
Story by James Nadwa