Kinamama wajane kutoka eneobunge la Mumias Mashariki wanalalamikia
kutengwa na vyiongozi wa eneo hilo
Kinamama hao Sasa wanasema kuwa hali ngumu ya maisha imewapa changamoto
wakitaka vyongozi kuingilia kati
Aidha wamelalamikia kulemewa na mzigo wa Karo wakati huu wanafunzi
wanaporejelea masomo baada ya msimu wa Corona
Haya yanajiri huku idadi ya juu ya kinamama wajane ikihofiwa kuongezeka
eneo hilo huku 3 Kati ya familia 5 zikiwa za wajane
Duru za kuaminika zadokeza kuwa kinamama hao hawanufaiki kwa vyovyote
na msaada kutoka kaunti ya Kakamega na hata serikali kuu juhudi zetu
kuzungumza na maafisa husika zikigonga mwamba
Story by James Nadwa