Lubao FM | 102.2 Hz

Wanasiasa eneo bunge la Mumias Mashariki

Mwanasiasa kutoka Wadi ya Makunga Malaha Isongo eneobunge la Mumias
Mashariki Peter Mango amelaumu uongozi kuwa chanzo Cha kufeli kwa
maendeleo katika Wadi hiyo

Kwenye mahojiano ya kipekee na waandishi wetu Mango amelalamikia ubovu
wa barabara pamoja na miundomsingi akisisitiza kuwa pana haja ya
kubanduliwa kwa uongozi katika Wadi hiyo

Amehoji kuwa hili pekee ndilo litakalowezesha kuimarika kwa Wadi hiyo
kimaendeleo

Kuhusu BBI Mango ametofautiana na kipengee kwenye mswada huo
kinachoruhusu kuondolewa kwa MCA na chama chake iwapo atafeli kufwata
masharti ya chama na hata serikali

Amesema kuwa hili litauwa demokrasia na kuleta udikteta kisiasa

Haya yanajiri tukiwepo na Sintofahamu kwenye zoezi la kuchapisha sahihi
zilizosanywa hivi maajuzi huku vuta nkuvute ikishuhudiwa Kati ya IEBC na
baadhi ya vyama vya kisiasa kuhusu zoezi hilo

Story by James Nadwa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE