Serikali ya kitaifa imetakiwa kuweka mikakati kabambe kwenye yaasisi zote za elimu nchini kama njia moja wapo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza baada ya kukabidhi mahema kwa vikundi vya akina mama katika eneo bunge la malava mwakilishi wa akina mama kaunti ya kakamega bi elsie muhanda amedokeza kuwa ipo haja kwa serikali kujitokeza na kutoa mahema kwa taasisi zote za elimu ili kutatua swala la uhaba wa madarasa unaoshuhudiwa katika shule kote nchini.

Mwakilishi huyo aidha amewarai walimu pamoja na wazazi kuwapa wanafunzi ushauri nasaha kuhusu umuhimu wa kurejelea masomo hasaa baada ya wao kupitia changamoto mbalimbali tangu kuripotiwa kwa virusi vya corona nchini.

Muhanda vilevile ametumia fursa hiyo kuwarai walimu wakuu  kuwapa wazazi muda wa kutosha  kuweza kulipia karo ya wanao shuleni.

Story by sajida javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE