Masaa machache baada ya serikali kufunga watu kutoingia na kutoka kwenye kaunti tano nchini ikiwemo kaunti ya Nairobi na pia kupandisha bei ya mafuta wahudumu wa magari za abiria kaunti ya Kakamega wakiongozwa na Everlyne Were mkurugenzi wa chama cha ushirika na mikopo cha magari ya matatu cha Hamazon wamelalamikia hatua hiyo wakisema kuwa imeathiri pakubwa biashara yao na kuusuta utawala wa rais Uhuru Kenyatta kwa kugandamiza hiyo.

Wakizungumza maeneo ya mayoni eneo bunge la Matungu, Bi Everlyne Were ambaye pia ni mmiliki wa matutu za Yesu ni Bwana ameisuta serikali kwa kuwagandamiza wafanyibiashara  na wakenya kwa jumla kwa kuzuia watu kuingia na kutoka kaunti ya Nairobi ambayo ni kitovu cha uchumi.

Kulingana na bi Were anataka serikali kutafuta njia mbadala ya kuzuia msambao wa virusi vya corona ikiwemo kuwapa  wakenya wote chanjo dhidi ya corona badala ya kufunga nchi.

Ni kauli iliyotiliwa mkaso na wahudumu wengine wa matatu ambao wamesema kuwa tayari wameegeza magari zao kusafirisha abiria kwa kushindwa kugharimia bei ya mafuta na masharti magumu yaliyowekwa na serikali kuendesha biashara hiyo.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE