Wenyeji wa kijiji cha mugai eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega
wameshangazwa na kisa ambapo mtoto wa miezi mitano amepatikana kwa boma la
mzee Beneya  Matsakha usiku wa kuamkia leo huku duru za kuaminika zikiarifu
kuwa mtoto huyo alitupwa na mwanafunzi wa darasa la nane mwenye umri wa
miaka kumi na nne.

Akizungumza na kituo hiki mzee Beneya amehoji kuwa  alirauka kuenda nje
kujisaidia saa nne za usiku ambapo alikutana na mtoto aliyekuwa amefungwa
kwa kitambaa kabla ya kuijuza familia yake nzima iliyomuokoa mtoto huyo.

Kwa upande wake Mildred Khatambi ambaye ni mamake mwananafunzi huyo amedai
kuwa mmewe Philip Mattsakha ndiye aliyemtunga mimba ya mapema mtoto huyo
huku juhudi za kutafuta haki kutoka kituo cha polisi cha Kabras zikiambulia
patupu akihoji kuwa kwa sasa anaishi kwa hofu tangu kisa hicho kutendeka.

Ni kauli inayoungwa mkono na Charles Jomo anayeonekana kuilaumu idara ya
usalama kwa kile anadai imetepetea katika juhudi za kumchukulia sheria
mshukiwa wa kisa hicho.

Hata hivyo familia hiyo inadai kuwa huenda mshukiwa alishirikiana na
mwaathiriwa ili kupoteza ushahidi wa kutambua babake mtoto huyo huku
mwanafunzi huyo akitoweka bila kujulikana aliko kwa sasa.


Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE