Chuo cha utabibu cha Kocholia Teso kitakuwa cha kwanza kuanzisha masomo ya utabibu mashinani [C.H.A] Community Health Assistant, wahudumu watakaopokea mafunzo hayo wakitumwa nyanjani kushughulikia magonjwa chipuka.
Haya yamesemwa na mbunge wa Teso kaskazini Dakt. Edward Oku Kaunya wakati wa maombi kwa takribani wanafuzi 150 watakao jiunga na chuo hicho kuanzia leo Jumatatu.
Kaunya amesema hazina ya NG,CDF Teso kaskazi imetoa ufadhili wa shilingi milioni 15 kwa wanafunzi hao 150 huku wanaotoka kwa familia yenye mapato ya chini wakilengwa.
Mbunge huyo ambaye amesema tayari hazina hiyo imetumia milioni 43 kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa chuo hicho, ikipania kuongeza milioni 30, ameongeza kuwa serikali ya kitaifa imeahidi milioni 12 kujenga makazi ya wanafunzi huku akitoa changamoto kwa jamii ya eneo hilo kujenga zaidi kwa manufaa yao.
By Hillary Karungani