Walimu katika Kaunti ya Bungoma ambao ni wanachama wa chama cha ushirika cha Metropolitan wametishia kujiondoa kutoka chama hicho kufuatia madai ya kunyanyaswa na kupewa viwango vya chini vya riba licha ya kuwekeza pakubwa katika chama hicho.

Huyu hapa mmoja walimu katika chama hicho akielezea masaibu wanayopitia walimu ambao ni wanachama wa Metropolitan.

Kwa sasa walimu hao wanaiomba miungano ya walimu KNUT na KUPPET kuwatetea walimu ambao ni wanachama wa chama cha ushirika cha metropolitan huku wakipendekeza kupewa pesa zao ili wawekeze kwingine.

Malalamishi haya yanajiri wakati chama hicho kimeandaa mkutano wa wanachama wake kitaifa kwa njia ya mtandao kwa kuzingatia kanuni za wizara ya afya kuzuia msambao wa virusi vya Covid-19.

Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE