Zaidi ya akina mama elfu moja kutoka vijiji vya Mechimeru, Sang’alo, Namwacha na Bulondo katika eneo bunge la Kanduyi Kaunti ya Bungoma ni miongoni mwa wale ambao wamenufaika na ufadhili wa mbegu ya mahindi aina ya Hybrid 513 kutoka kwa vuguvugu la Bungoma Liberation msimu huu wa upanzi.

Akizungumza wakati wa kuzindua mpango huo wa utoaji mbegu hiyo, Isaiah Sakonyi ambaye ni mshirikishi wa vuguvugu hilo eneo bunge la Kanduyi, amesema nia yao ni kuzifikia familia zenye mapato ya chini na zilizokosa kupata ufadhili wa mbegu kutoka kwa serikali ya Kaunti.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE