Muungano wa walimu wa shule za upili KUPPET katika kaunti ya Kakamega unaitaka wizara ya elimu kugatua zoezi la kusahisha mitihani ili kuepusha mchanganyiko wa walimu wa kusahisha mtiahani kutoka sehemu mbali mbali na kuhatarisha maisha yao kwa maambukizo ya corona
Katibu wa muungano huo Harrison Otota pamoja na mwenyekiti Johnston Wabuti wanawataka walimu kutokubali kushurutishwa kuenda jijini Nairobi kwa zoezi la kusahisha mitihani
Wakati uo huo Wabuti ameitaka serikali kutowashurutisha walimu kupokea chanjo ya corona kabla ya kuchaguliwa kusahisha mitihani
By Richard Milimu