Jamii ya waislamu mjini Kakamega na vyunga vyake sasa inaitaka serikali kupitia kwa idara ya ardhi kuwapa hati miliki ya kipande cha ardhi ambako msikiti mkuu wa Kakamega umejengwa mjini humo.
Wakiongea mjini Kakamega baada ya kuchaguliwa kama viongozi wapya wa msikiti wa jamia Kakamega, mwenyekiti mpya Kassim Hassan na kiongozi wa wanawake waislamu Marriam Andati wamesema tangu mwaka wa 1973 walipopewa ardhi hiyo na serikali bado hawana stakabadhi rasmi za umiliki.
Wanasema hali hiyo imekuwa ikizuia kutekelezwa kwa shughuli nyingi za maelfu ya waislamu mjini humo.
Wakati uo huo wazee waislamu wamepongeza kamati mpya simamizi ya msikiti huo ambayo imechaguliwa, wakiwataka kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Jinsi anavyoeleza mzee Ramadhan Yaku
By Richard Milimu