Wakaazi wa kijiji cha Bukhakunga,wadi ya Kabras Kusini,eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wametakiwa kuzingatia sheria za kudhibiti msambao wa virusi vya corona
Ni kauli yake mzee wa kijiji wa sehemu hizo Stephen Muhongo Isindu akizungumza na kituo hiki baada ya mazishi ya aliyekuwa mwalimu Semeo Mugami mapema hii leo
Stephen amelalamikia wizi wa mahindi na miwa katika kijiji hicho na kuwatahadharisha wakaazi wake dhidi ya kutojihusisha na wizi
Amewataka wazazi pia kuhakikisha wanao wanaenda shule bila kuketi nyumbani akisema mzazi atakayekosa kumpeleka mwanawe shuleni atakabiliwa na mkono wa sheria
By Sajida Javan