Mwanafunzi mmoja kutoka Kaunti ya Kakamega na anayeishi eneo bunge la Kimilili kaunti ya Bungoma amewashangaza wengi baada ya kutembea zaidi ya kilomita Kumi hadi shule ya upili ya wavulana ya Teremi ili kujisajili kwenye kidato cha kwanza huku akiwa bila chochote hitajika.ila barua ya usajili wa shule ya teremi pekee.
Mwanfunzi huyo Stephen Otawa ambaye ni yatima anasema kuwa amekuwa akisomea katika shule ya watoto yatima iliyoko Kimilili na kufaulu kupata alama 355 kwenye mtihani wa KCPE mwaka 2020.
hata hivyo kutokana na ufukara,hajaweza kujiunga na kidato cha kwanza baada ya Nyanyake aliyekuwa akimtegemea kufariki dunia mwezi uliopita.
Akithibitisha kumpokea mwanafunzi huyo, Naibu Mwalimu Mkuu wa shule hiyoWanyama Munoko amesema mwanafunzi huyo anahitaji msaada kutoka kwa wahisani ili kufanikisha masomo yake, huku shule hiyo ikiwa tayari imeanzisha mchakato wa kumsajili shuleni humo.
Kwa sasa wito unatolewa kwa wahisani kumsaidia mwanafunzi huyo anayetoka eneo bunge la Navakholo Kaunti ya Kakamega kupata ufadhili aendeleze masomo yake.
By Hillary Karungani