Wakaazi wa eneo la Chwele eneo bunge la Kabuchai Kaunti ya Bungoma sasa wameitaka idara ya afya kwenye Kaunti hiyo kuingilia kati na kuangazia kile wanachodai ni wizi wa dawa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kabuchai huku wagonjwa wakizidi kutaabika kufuatia uhaba wa dawa.
Baadhi ya wale tuliozungumza nao wanasema wanaagizwa kununua dawa nje ya hospitali kwa gharama ya juu.
Kwa sasa wametoa makataa ya siku 14 kwa serikali ya Kaunti ya Bungoma kupitia idara ya afya kutafuta suluhu ya kudumu la sivyo watashiriki maandamano kushinikiza kutimuliwa Daktari msimamizi wa hospitali ya Kaunti ndogo ya Kabuchai.
By Hillary Karungani