Vitengo vya usalama katika kaunti ya Bungoma vimetakiwa kuingilia kati upesi na kusitisha visa vya utovu wa usalama ambavyo vinaendelea kushuhudiwa.

Haya ni kwa mujibu wa mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu Derick Wauswa Wafula, ameelezea kusikitishwa na ongezeko la visa vya mauaji ya kiholela huku akitoa wito kwa idara ya usalama katika kaunti ya Bungoma kuwatia nguvuni  wahalifu wanaoendeleza uovu huo.

Wakati uo huo Wafula amependekeza kupewa uhamisho  maafisa wa polisi waliohudumu eneo hili kwa muda mrefu akidai kuwa wametelekeza  majukumu yao kando na kuendeleza dhulma kwa wananchi haswa wanapotekeleza amri ya kutopatikana nje.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE