Hatua ya baadhi ya wazazi kaunti hii ya Bungoma kutowajibikia majukumu yao ipasavyo  imetajwa kuchangia ongezeko la visa vya mimba za mapema miongoni mwa watoto wasichana.

Akihutubu kwenye hafla ya kuwahamasisha wakaazi wa wadi ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon  kuhusu athari za mimba za mapema miongoni mwa wasichana , chifu wa kata ya Cheptais bi. Vellah Chebus ametaja ukosefu wa mazunguzo kati ya wazazi na wanao kama mojawepo ya sababu, zinazochangia  mimba za mapema miongoni mwa wasichana wadogo.

Naye mwenyekiti wa walimu wakuu wa shule za msingi kaunti ndogo ya Cheptais bi  Catherine Kones amehoji kuwa uuzaji wa pombe haramu, imechangia ongezeko la visa vya mimba za mapema ambapo amewasihi wananchi kujitenga na biashara hiyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa walimu wa kike kwenye muungano wa kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT tawi la Mlima Elgon bi Jemimah Temko, akiwataka wazazi kuwapa wanao mahitaji ya kimsingi kando na kuwalea kwa misingi ya kidini.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE