Wito unazidi kutolewa kwa wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwapa familia moja kutoka kijiji cha Matibo, kata ya Namwela eneobunge la Sirisia msaada wa kifedha utakaowawezesha kugharamia ada ya matibabu ya mwaname.

Haya ni kwa mujibu wa bi. Judith Lwala ambaye anahoji kuwa mwanawe Philip Wanjala Masinde mwenye umri wa miaka thelathini na nane, baba wa watoto watatu alihusika kwenye ajali barabarani jijini Nairobi mwezi wa tano mwaka huu ambayo ilimwacha na majeraha ya kichwa, ambapo amewataka wahisani na viongozi wa kaunti hii ya Bungoma kumpa usaidizi wa kifedha ili kugharammia ada ya shilingi elfu mia moja hamsini itakayofanikisha upasuaji wa kichwa.

Aidha bi. Lwala anasema iwapo atapokea msaada huo utamwezesha kumpeleka mwanawe afanyiwe upasuaji wa kichwa ili kumwondolea uchungu na maumivu anayopitia kwa sasa.

Awali kwenye mahojiano na wanahabari nyumbani kwao Matibo, Philip Wanjala Masinde alionekana kuzidiwa na maumivu ambapo alidokeza kuwa imefika wakati ambao alikuwa ameanza kukata tamaa ya kupata usaidizi huo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE