Uozo unazidi kushuhudiwa kwenye masoko mabalimbali nchini huku wafanyibiashara wakitatizika kutokana na mazingira machifu ya kuendeshea biashara zao

Katika soko la Harambee eneobunge la Matungu wafanyibiashara sasa wanahofia mkurupuko wa wagonjuwa 

Wafanyibiashara hao wanaitaka serikali ya kaunti kushugulikia swala hilo haraka iwezekanavyo kwani wanatozwa ushuru kwa kiwango cha juu

Katika soko la Makunga eneobunge la Mumias Mashariki mambo ni yale yale huku wafanyibiashara wakilalamikia ukosefu wa maji huku pamoja na vichaka ambavyo wanadai vimewaogofya na kuwafurusha sokoni humo

Haya yanajiri siku kadhaa baada ya nyuki kumvamia na kumjeruhi mfanyibiasahara mmoja na sasa wanahofia usalama wao

Akizungumza na kituo hiki mshauri wa maswala ya uongozi katika serikali ya kaunti ya Kakamega Ali Musa Chibole amekiri kuwepo na tatizo hilo ila akasema kuwa linatafutiwa suluhu ya kudumu

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE