Waziri wa elimu profesa George Magoha Amedhibitisha kuwa wanafunzi wa shule za msingi na za upili  watalazimika kurejelea masomo mwaka ujao. Aidha ni watahiniwa wa darasa la nane na wa kidato cha nne tu watakaorejea darasani Septemba mwaka huu japo hawatafanya mitihani ya KCPE na kcse mwaka huu.

Akitangaza kalenda mpya ya shule hii leo waziri wa elimu profesa George Magoha anasema serikali imelazimika kuzuia masomo kuendelea kutokana na tishio la maambukizi ya virusi vya corona.

Hata hivyo vyuo vikuu vimeruhusiwa kurejelea masomo na kwa kuzingatia kikamilifu masharti ya kudhibiti virusi vya corona.

Uamuzi wa waziri wa elimu Magoha umeungwa mkono na katibu mkuu wa chama cha walimu Wilson Sossion akiwataka wazazi kuwa waangalifu kuhusu mienendo ya wanao ili kuwaepusha kuambukizwa virusi vya corona wakiwa nyumbani.

Waziri wa elimu profesa George Magoha amedokweza kuwa shule zote zitahitajiwa kuwa na sehemu za kunawa mikono pamoja na kuwawezesha wanafunzui  kudumisha umbali wa mita moja unusu.

Waziri Magoha kadhalika amekiri kuwa serikali itahitajiwa kuongeza idadi ya walimu hasaa katika shule za upili ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kutokana na mabadiliko yatakayotekelezwa.

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE