Vijana wanaojihusisha na wizi wa vyuma kwenye daraja eneobunge la Lurambi vyuma vyao vi motoni baada ya mbunge wa eneo hilo askofu Titus Khamala kusema wataanzisha msako mkali kwa ushirikiano na idara ya usalama ili kuwatia mbaroni wahalifu…
Kupitia kwa mwakilishi wake Daniel Kadenge akiwahutubia waombolezaji katika hafla ya mazishi maeneo ya Shikhambi wadi ya Sheywe , askofu Khamala anasema vijna wengi kutoka wadi za Shirere,Sheywe na Mayakalo haswa mitaa ya Shikhambi,Amalemba na Jua Kali wanaojishuhusisha na wizi wa vyuma kwenye daraja katika eneobunge hilo kando na kuwaangaisha wakazi nyakati za usiku wamewekewa mtego na lazima utawanasa
Mbunge huyo aidha ameihakikishia shule ya msingi ya Nabongo na ile ya Maraba madarasa mengine jinsi alivyofanya katika shule zingine kama njia mojawapo ya kuinua hathi ya masomo eneobunge lake kwa kuwapa wanafunzi na walimu mazingira mazuri ya kusomea
Kwa upande wake Gilbert Alushula mmoja wa wanasiasa aliyekuwa miongoni mwa waombolezaji, amesikitikia hatua ya serikali kutishia kuwashika wazazi ambao wanao hawajajiunga na kidato cha kwanza akidai wengi wa wazazi wamesalia katika njia panda baada ya kukabwa koo na lindi la umasikini.
By Lindah Adhiambo