Shule ya upili ya Mukhweya eneo bunge la Matungu imenufaika na ufadhili wa madarasa mawili kutoka kwa muungano wa wasomi katika wadi ya Kholera maarufu kama Kholera Professionals kwa kima cha shilingi nusu millioni
Mwenyekiti wa muungano huo Emmanuel Makokha amesema ni ufadhili kutoka kwa mifuko yao kama njia ya kurudisha mkono kwa jamii
Wamewahimiza wenzao kujitokeza kuungana nao kukuza jamii
Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Mukhweya Colleta Were amepongeza msaada huo na kuwataka viongozi kuunga mkono
ni usemi uliosisitizwa na mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Edwin Buluma
By Lindah Adhiambo