Huku Padre Mkuu  Wa Kanisa  la Katoliki Parokia kuu ya  Bungoma (Christ the King)  Fr Wanyonyi anatilia Shaka   Chanjo ya Covid_19 ,inayoendelea kupeanwa kote Nchini hali inayozua mtafaruku.

Padri wa Kanisa la K.A.G(Bungoma) Edward Wekesa ameitilafiana vikali  na msimamo huo huku akiutaja kama usiofaa kabisa. Askofu Wekesa  amesema kuwa kama kanisa lazima waonyeshe mfano mzuri na  wafuate kanuni za serikali na kuimiza washiriki  wao kupewa chanjo.

Kwenye mkao na wanahabari Ofisini mwake,Askofu Wekesa  amelezea Imani yake kuhusiana na Chanjo yenyewe huku akiomba umma kuikumbatia kwa minajili ya afya yao.

Kuhusiana na marufuku dhidi ya mikusanyiko, Askofu Wekesa amewaomba wanasiasa kukumbatia agizo hilo la serikali huku akisema kuwa itapunguza msambao zaidi wa virusi  hivyo hatari vya Korona.

Kuhusiana na likizo hii ndefu ya wanafunzi Askofu Wekesa  amelezea kuisikitikia mienendo ya baadhi ya wanafunzi huku akiwatahadharisha wazazi dhidi ya kuwadegeza wanao.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE