Ni ujumbe heri wa heri njema ya Pasaka kwa wakristo kutoka kwa mshauri na kasisi wa kanisa la Full Gospel Assemblies of Kenya Nashon Otwane.
Kwenye mkao na wanahabari ofisini mwake , kasisi Otwane amesikitikia namna vijana haswaa wa umri mdogo wanavyojiingiza kwa madawa ya kulevya huku akinyoshea kidole cha lawama baadhi ya wazazi kwa mienendo inayochangia uovu huo.
Kasisi Otwane ametilia shaka mienendo haswaa ya baadhi ya wazazi kubugia tembo kupita kiasi huku akisema kua inachochea wanao kuiga mitindo hiyo.
Aidha kwa mara nyingine kasisi huyo amewahimiza wakristo kuwa na moyo wa msamaha na maridhiano kama njia moja ya kuonyesha upendo kwa yesu kristo huku akisema kua ndio njia ya pekee itakayoikomboa nchi kutokana na majanga.
Ikumbukwe kua wakristo kote duniani wanasherehekea kufufuka kwa yesu kristo kwa mara ya kwanza sherehe hizo zikifanyika kote nchini chini ya masharti makali yaliyowekwa na wizara ya afya kuhusiana na covid-19 huku wengi wa wakristo wakiadhimisha sherehe hizo nyumbani.
By Hillary Karungani