Kama njia mojawapo ya kuendeleza ukulima kwa kupitia kwa makundi na mashirika mbali mbali nchini, sasa vijana kutoka waliojiunga kwa pamoja na kujiingiza katika ukulima  kutoka Butsotso Mashariki, eneo bunge la Lurambi wamebahatika kupata ufadhili kutoka kwa shirika la Kenya Climate Smart Agriculture Project( KCSAP) wa shilingi 874,000 .

Akizungumza na idhaa hii akiwakabidhi pembejeo hizo kwa njia ya kipekee, Jennifer Awino amewahimiza vijana kujiunga kwenye makundi na kuanzisha miradi endelevu itakayo wakwamua kutoka kwenye lindi la umaskini.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Livingstone Youth Group Sizianne Lilumbi pamoja na mlezi wao mama Caroline Lilumbi hawakuweza kuificha furaha yao huku wakiaidi kuzitumia vilivyo pesa hizo.

Kwa upande wake afisa wa kilimo biashara kutoka Butsotso Mashariki Humphrey Matheshe anasihi serikali za kaunti na kitaifa kuendelea kuegeza kwenye vijana kwa kuweka viwanda na pesa za ufadhili.

Mzee wa nyumba kumi wa sehemu hiyo ya Emusala ametoa onyo kali kwa yeyote atakaye jaribu kuiba vifaa hivyo, samaki au kuku.

Ufadhili huo wa shilingi  874, 000 kutoka kwa  KCSAP umekezwa katika kilimo cha samaki pamoja na ufugaji wa kuku kwenye kikundi hicho cha Livingstone Youth Group chenye vijana kumi na saba.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE