Sehemu za ibada katika kaunti ya Kakamega zilishuhudia idadi ndogo ya waumini kuadhimisha Ijumaa kuu huku wengi wakisalia manyumbani kwa sababu ya masharti ya corona

Maandamano ya kawaida ya waumini wa Kanisa katoliki kuadhimisha Mafumbo ya Mateso ya bwana yesu kristo hayakufanyika huku ibada zikiwa na unyamavu

“ leo ni siku ambayo wakrito huja kanisani kwa wingi ili kuweza kuadhimisha siku hii ya ijumaa kuu. Mwaka huu na mwaka jana watu wajaweza kuadhimisha siku hii kwa mandamano ya njia ya msalaba. Siku ya leo tuombe rehema za mwenyezi Mungu ili tuweze kushinda mauti ya virusi vya corona jinsi yesu alishinda mauti ya kifo.”

Hata hivyo baadhi ya wakazi wamelalamikia hali ngumu ya maisha kutokana na masharti magumu ya corona ambayo hata yamewazuia kwenda kanisani

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE