Huku taifa la Kenya likiungana  na ulimwengu kuadhimisha siku kuu ya pasaka viongozi wa kidini katika kaunti ya Bungoma wametoa wito kwa wakristo kuliombea taifa hili hasa wakati ambapo linakumbwa na janga la korona na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu nchini.

Wakizungumza na wanahabri   mjini Webuye viongozi hao wakidini wakiongozwa na mwenyekiti wa ushirika wa Webuye Alex Masika na mweyekiti wa wahubiri  eneo bunge la Webuye Magharibi David Walukhu wamesikitikia mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu humu nchini wakisema kuwa mwananchi wa kawaida anapitia hali ngumu huku wakiwataka wakristo kutumia fursa hii ya pasaka kuombea taifa hili.

Viongozi hao wa kidini hata hivyo wamewashutumu wanasiasa kwa wimbi la pili la janga la korona wakisema wao ndio walichangia kuongezeka kwa idadi ya maambukizi na  vifo kwa kupuuza masharti ya wizara ya afya kwa kuandaa mikutano ya hadhara huku wakiwataka wazazi kuwalinda wanao wakati huu wakiwa nyumbani kwa likizo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE