Huku Padre Mkuu Wa Kanisa la Katoliki Parokia kuu ya Bungoma (Christ the King) Fr Wanyonyi anatilia Shaka Chanjo ya Covid_19 ,inayoendelea kupeanwa kote Nchini hali inayozua mtafaruku.
Padri wa Kanisa la K.A.G(Bungoma) Edward Wekesa ameitilafiana vikali na msimamo huo huku akiutaja kama usiofaa kabisa. Askofu Wekesa amesema kuwa kama kanisa lazima waonyeshe mfano mzuri na wafuate kanuni za serikali na kuimiza washiriki wao kupewa chanjo.
Kwenye mkao na wanahabari Ofisini mwake,Askofu Wekesa amelezea Imani yake kuhusiana na Chanjo yenyewe huku akiomba umma kuikumbatia kwa minajili ya afya yao.
Kuhusiana na marufuku dhidi ya mikusanyiko, Askofu Wekesa amewaomba wanasiasa kukumbatia agizo hilo la serikali huku akisema kuwa itapunguza msambao zaidi wa virusi hivyo hatari vya Korona.
Kuhusiana na likizo hii ndefu ya wanafunzi Askofu Wekesa amelezea kuisikitikia mienendo ya baadhi ya wanafunzi huku akiwatahadharisha wazazi dhidi ya kuwadegeza wanao.
By Hillary Karungani