Mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake eneo bunge la Lurambi bi Agnes Barasa amewahimiza wenyeji haswa akina mama kujiunga kwenye makundi na kutumia mvua inayonyesha kwa sasa kupanda vyakula vinavyochukua muda mfupi kama njia moja ya kukuza uchumi wa sehemu hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano uliowaleta pamoja akina mama wajane kule Lurambi kuwahamasisha njia za kutoka kwenye uchochole,bi Barasa ametaja kuweko kwa soko la kutosha kwa vyakula hivyo na kuwataka kutumia fursa hiyo kujikamua kutoka katika lindi la uchochole.
Wakati huo uo kiongozi huyo amewataka akina mama hao kupanda mboga za kienyeji kwa wingi za kuuza na kutumia akisema kuwa ni tiba ya mwili .
By Richard Milimu