Siku chache tu baada ya mfadhili almaarufu Devki kujitokeza kutaka kuwekeza ili kukifufua kiwanda cha sukari cha Mumias, wakulima wa miwa katika eneo hilo wamelalamikia kutohusishwa katika mpango huo. 

Wakizungumza mjini Mumias kaunti ya Kakamega wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa chama cha wakulima wa miwa Simon Wesechere wakulima hao wamelalamika kutohusishwa katika mpango wa kufufua kiwanda hicho ilhali wao ndio washikadau wakuu huku wakiitisha kikao cha kukusanya maoni ya umma na mweka hazina huyo ili kupeana maoni yao.

Wakulima hao aidha wameitaka serikali kujitokeza wazi na kuelezea ni wapi watatoa miwa ilhali wakulima zaidi ya elfu 40 walijitoa katika ukulima wa miwa na kujiunga na ukulima wa miwa huku wakiitaka kuhakikisha kuwa wanaweka mipango dhabiti kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi milele

Wakati uo huo wamemtaka meneja anayesimamia kiwanda hicho kwa niaba ya benki ya KCB kuweka wazi ripoti kamili ya fedha wanazopata ili kujua kiwango cha deni ambacho kiwanda hicho kimebakisha kulipa. 

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE