Hazina ya ustawishaji maendeleo ya CDF eneo bunge la Lurambi imeanza upeanaji wa fomu za basari kwa wanafunzi kutoka jamii maskini ili kuendeleza elimu yao katika shule za upili,vyuo vikuu na taasisi za kadiri.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika afisi za hazina ya CDF ya eneo bunge la Lurambi zilizoko mjini Kakamega, mbunge wa eneo hilo askofu Titus Khamala amesema kuwa fomu hizo elfu sita zitapeanwa kwa machifu na manaibu wao ambapo watapeana kwa wanafunzi kutoka jamii maskini pekee kuzijaza kisha kuzirudisha kwa afisi za machifu hao.
“tunataka kupeana forms za bursaries kwa watoto ambao hawajiwezi wa shule za upili, universities, polytechnics na ata special schools.” Alisema mbuge huyo
Kulingana na khamala anasema kuwa hapo awali wanafunzi kutoka jamii zenye uwezo zilikuwa zikipata pesa hizo kupitia kwa matapeli na mtindo huo mpya utazuia wanafunzi kutoka familia zenye uwezo kunufaika na badala yake kunufaisha wale kutoka familia maskini.
“hizi forms tutapeana kwa ukweli ili pia wale ambao hawajiwezi waweze kusoma. Kwa wale mko na uwezo tafadhalimuachie wale hawajiwezi.”
Hata hivyo mbunge huyo amehoji kuwa hakuna pesa zozote zilizotolewa mwaka jana kugharimia karo ya wanafunzi kutokana na mkurupuko wa janga la corona na kusema kuwa pesa hizo zilielegezwa kwenye ujenzi wa madarasa.
story by Lihavi IMelda