Ili kufanikisha juhudi za wizara ya elimu kwa maswala ya miundo msingi katika shule za umma humu nchini, mwakilishi wadi wa Sabatia Magharibi ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Vihiga Henry Asava ,sasa ameanzisha mpango maalum wa kuchangisha pesa za upanuzi wa baadhi za shule  eneo hilo zenye changamoto ya manthari bora kwa wanafunzi.

Akizungumza baada ya kuchangisha pesa za shule ya upili ya Kegondi kupitia chakula maalum katika mkahawa wa Hemara mjini Chavakali,Asava amesema kuwa mpango huo ndio njia pekee ya kuokoa hali ya manthari ya masomo kwa wanafunzi ikizingatiwa changamoto ambazo wizara hiyo inapitia katika kufanikisha mipangilio yao haswa msimu huu  wa janga la covid-19.

Matamshi hayo yameungwa mkono na mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Bw.Bob Busungu na mwalimu wa shule hiyo Bi.Josephene Zindoli ambao wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama wa wanafunzi hao na kwamba ipo haja ya wadau zaidi kujitokeza ili kufanikisha shughuli hio.

Pia miongoni mwa shule zinazolengwa eneo hilo ni pamoja na Galoni, Chandumba na Serelwe .

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE