Chama cha UDA kimeweka  wagombea wake mbalimbali ambao watagombea vyeo mbalimbali kupitia tiketi ya chama hicho. Katika eneo bunge la Kabuchai, Evans Kaikai ameteuliwa kuipeperushia bendera ya Chama hicho. Katika kata ya Huruma, Kelele Nelson ndiye mgombea na huku Bernard Muia kiala akigombea kama seneta wa kaunti ya Machakos.

Katika kikao kilichofanyika hii leo kikiongozwa na mwenyekiti Johnson Muthama, Margaret Wanjiru ametajwa kama mgombea wao kaunti ya Nairobi katika uchaguzi mdogo ujao.

Wakati wa matangazo ya wagombea hao, viongozi  wanaoshirikiana na naibu rais pia walikuwepo wakiongonzwa na Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na pia seneta Susan Kihika wa Nakuru. Wengine ni Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wa ,Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagwa,Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri  na wengineo.

Ikumbukwe kuwa uteuzi  huu unakuja siku baada ya chama cha UDA  kujisajili  kama chama rasmi cha kisiasa.

Story by Lavine Wanzetse

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE