Wauguzi wamsihi Rais Uhuru Kenyatta kusuluhisha mzozo katika sekta ya afya. Katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha wauguzi, Seth Panyako amesema mazungumzo yaliyonuiwa kumaliza mgomo wa wauguzi wa mwezi mmoja yanapuuziliwa na maafisa wa serikali ya kitaifa na zile za kaunti.

Katibu huyo mkuu anasema magavana wamekataa kutia saini mkataba wa makubaliano ya kurejea kazini.

 “Baraza la Magavana limekataa kutia saini utaratibu wa kurejea kazini likidai halikushauriwa. Huo ni uwongo mtupu. Baraza hilo liliwakilishwa wakati wote wa majadiliano.” Amesema panyako

Hii leo panyako akizungumza na wanahabari amepuzilia mbali madai ya serikali za kaunti kwamba  hazina fedha za kufadhili utaratibu wa kurejea kazini.

“Serikali ya kitaifa imekubali kufadhili mpango wa kurejea kazini. Swala eti serikali za kaunti hazina fedha ni potovu,”  panyako alieleza.

Wauguzi  humu nchini wamegoma kwa muda wa siku 32 na wameelezea kuwa watasimama kitede na kuendelea na mgomo hadi makubaliano yatakapo afikiwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE