msichana wa umri mdogo aliyekuwa chini ya utunzi wa kaasisi mmoja wa Kanisa la Legio Maria, sasa familia yake inataka kaasisi huyo kukamatwa kwa maadai ya kampachika mimba katika kijiji cha komenya kaunti ya Siaya.

William Wasonga mwenye umri wa miaka 74, na Mwalimu wa dini katika Kanisa la Legio Maria la St Marys Nyahombe , anadai kwamba kasisi huyo alimpachika mimba mjukuu wake na kumharibia maisha na pia ni tisho kwa waschana wengine wa Kanisa hilo.

Wasonga aliyeandamana na mjukuu wake aliye na mimba ya miezi mitano, Akizungumza na wanahabari humu nchini,    alisema familia ilipashwa habari na marafiki kwamba msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 na ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu alikuwa mja mzito.

Kulingana na Wasonga kasisi huyo alikubali alimpachika mimba michana huyo na hata akatuma shilingi 4,500 za kufadhili msichana huyo kuavya mimba.

Hata hivyo, kasisi huyo, Ibrahim Omondi alithibitisha kwamba alikuwa anaishi na msichana huyo lakini akakanusha madai kwamba alimpachika mimba.

Kasisi huyo ambaye tayari amesimamishwa kazi kwa madai ya kukosa uadilifu alisema kwamba madai hayo yalikuwa njama ya kumchafulia jina na kumfurusha kutoka kanisa hilo kufuatia mizozo inayoendelea kanisani humo.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE