Cristiano Ronaldo aliandikisha historia kwa mchuano wake wa 600 wa ligi kwa kufunga bao la 20 katika Serie A msimu huu walipoishinda Spezia mabao matatu kwa nunge

Mabao yote matatu yalifungwa katika kipindi cha pili huku Ronaldo akilifunga goli la tatu alipotumia vyema fursa ya kupewa pasi katika dakika ya mwisho.

Alvaro Morata alikuwa amefunga bao la kwanza kutumia krosi ya mwenzake Federico Bernardeschi kabla ya Federico Chiesa kufunga goli la pili.

Ushindi huo sasa umeisongesha Juventus hadi alama tatu chini ya nambari mbili AC Milan katika Jedwali la Serie A .

Bao la Ronaldo sasa linamaanisha anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga takriban mabao 20 katika kila vipindi 12 vya ligi tano kubwa za bara ulaya.

Na kule Liverpool Meneja wa klabu  hiyo Jurgen Klopp anasema kwamba mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah ni mchezaji muhimu wa klabu hiyo na anatumai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atasalia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Story by Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE