Hatimaye mshindi wa uchaguzi mdogo wa kutoka wadi ya Huruma kaunti ya Uasin Gishu Lucy Ng’endo Chomba ametawazwa mshindi na tikiti ya chama cha Jubilee.

Kinyang’anyiro hicho kilikuwa na upinzani mkali kwani Lucy Chomba alipata ushindi na kura 2498 wapili akiwa Wanjohi Peter Kimani ambaye alipata kura 1147 na watatu akiwa Njoroge Francis Maina na kura 980.

Hata hivyo mshindi wa wakilishi wa wadi ya Huruma Lucy Chomba amewapongeza waliompigia kura na amehimiza wapinzani wake kuungana pamoja na kuendeleza kazi.

Lucy Ng’endo Chomba ni mke wa mwendazake Peter Chomba ambaye alikuwa mwakilishi wa wadi ya huruma aliaga mwaka 2020 tarehe 18 mwezi wa Oktoba.

Story by Sharon lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE