Wananchi wanashauriwa kuzingatia maswala na usafi wa vyakula wanapokuwa katika ibaada za mazishi.
Akiwahutubia waombolezaji katika ibaada ya mazishi ya mwenda zake James Wendo katika kijiji cha Lukusi-B kata ndogo ya Lukusi iliyo katika wadi ya Isukha Mashariki eneo bunge la shinyalu, naibu chifu stephen buhoya anawashauri wale wanaoandaa vyakula kuzingatia usafi.
vilevile anawahimiza wananchi kuzingatia sheria za covid-19 bila kupuuza.
Hata hivyo anawauliza wazazi kuzingatia mkataba waliouweka na walimu shuleni ili kuepusha wanafunzi kutumwa nyumbani badala ya kusalia darasani na kuzingatia masomo.
Ni ibaada iliyoendeshwa chini ya kanisa la muusa pag linaloongozwa na mchungaji rev. Wycliffe machacho chini ya askofu mwangalizi wa wilaya ya pag ivihiga – ileho rev. Vincent mukeiya.