Mwanaume mwenye umri wa makamo kwa majina Jullius Omboko kutoka kijiji cha Matsakha eneobunge la Malava kaunti ya Kakamega anasakwa na maafisa wa polisi baada ya kudaiwa kushiriki tendo la ndoa na mwanawe mwenye umri wa miaka 12.
Wakizungumza na idhaa hii wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na mzee wa mtaa Rose Musa wamehoji kuwa mwanaume huyo alianza kumtumia mwanae akiwa na chini ya umri wa miaka minane na kuadhiri maisha yake.
Kulingana na mshukiwa Jullius Omboko amedai kuwa mkewe alimtupa mtoto na kutorokea kwao jambo lililomlazimu achukuwe hatua ya kuishi nae.
Aidha naibu chifu wa eneo hilo John Chebsanyi amekerwa na kitendo hicho na kuwaonya watu ambao watapatikana wakishiriki tendo la ndoa na watoto wenye umri mdogo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.