Serikali ya Kaunti ya Trans-Nzoia imepokea miche 43,300 ya Parachichi na Miche 30,900 ya Makadamia kupitia kwa mpango wa wizara ya Kilimo kupiga jeki Kilimo mseto badala ya kutegemea Kilimo cha mahindi pekee.
Kwenye mkao na wanahabari wakati wa kupokea miche hizo waziri wa Kilimo Kaunti ya TransNzoia Bi Mary Nzomo ametoa changa moto kwa wakulima kukumbatia kilomo cha mimea hiyo, kwa kile ametaja kama njia moja wapo ya kupiga jeki uchumi wa wakulima Kaunti hiyo, mbali na kutoa hakikisho la soko mazao hayo.
Aidha Nzomo ametoa wito kwa wakulima wanaohitaji miche za parachichi, Makadamia,Chai,kahawa na Ndizi kutembelea maafisa wa kilimo nyanjani ilikupata mwelekeo wa kupokea miche hizo ambazo bei yao imepunguzwa na serikali ya Kaunti.
By Richard Milimu