Viongozi nchini wametakiwa kupunguza joto la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa nchini na badala yake kuhakikisha kuwa wanawafanyia kazi kikamilifu wananchi waliowachaguwa

Haya ni kwa mujibu wa mbunge wa Ikolomani Benard Shinali akizungumza kwenye hafla ya kufungua rasmi jengo la orofa la maktaba na maankuli katika shule ya upili ya Shichinji katika eneo bunge lake, ambapo amewarai viongozi kupunguza siasa hasa wakati huu ambapo nchi inakumbana na makali ya janga la corona

Shinali wakati uo huo amewataka wakaazi wa eneo bunge la Ikolomani kuwa waangalifu na watu wasiojulikana wanaokuja kwenye eneo hilo kwa madai ya kuchimba migodi ilhali wanaendeleza uhalifu. Hii ni baada ya visa vya uhalifu kuongezeka eneo hilo.

Shinali aidha amechukuwa fursa hiyo kuwapongeza walimu eneo hilo kwa matokeo bora ya  mtihani wa kitaifa huku mwalimu mkuu wa shule hiyo  Cassius Khatachi Lumwamu akiahidi matokeo bora zaidi mwaka huu.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE