Viongozi wa kisiasa kutoka eneo la Magharibi mwa nchi wamehimizwa kuweka tofauti zao kando za kisiasa  na badala yake kuongea kwa sauti moja na kushirikiana kikamilifu iwapo wanatarajia  kutwaa uongozi wa taifa hili kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Kolani eneobunge la Sirisia mwakilishi wa kike kaunti ya Trasnzoia Bi Janet Nangabo amesema migawanyiko  miongoni mwa wanasiasa wa jamii ya mulembe huenda ukawanyima fursa ya kuongoza taifa hili baada ya uchaguzi mkuu  ujao.

Aidha Bi Nangabo amependekeza kubuniwa chama kimoja cha kisiasa eneo la Magharibi  ili kusitisha  migawanyiko inayoshuhudiwa kwa sasa.

Amewataka wazazi kuwekeza kwenye elimu ya wanao ambayo amesema itawafaidi pakubwa siku za usoni.

Naye mwanaharakati wa kisiasa kaunti ya Bungoma Moses Waliaula akitaka kuwepo mazungomzo kati ya gavana wa kaunti hii Wycliffe Wangamati  na wawakilishi wadi ili kusitisha malumbano ya kila mara.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE