Wenyeji wa Kaunti ya Trans-Nzoia wanatarajiwa kufaidi msaada wa neti 600,070 ya kuzuia msambao wa mbu inayosababisha maradhi ya Malaria nchini.
Akihutubu kwenye mkutano wa hamasisho kwa washikadu katika sekta ya afya, waziri wa afya Kaunti ya Trans-Nzoia Bi Clare Wanayama amesema kaunti ya Trans-Nzoia inashuhudia 3% ya msambao wa malaria dhidi ya 8% kote nchini, akisema wizara yake inalenga kutoa matibabu kwa watakao ambukizwa malaria bila ya kupoteza maisha ya yeyote Kaunti hiyo.
Kwa Upande wake Dkt Philip Bett mkurugenzi wa maswala ya kukabili maambukizi ya malaria Kaunti ya Trans-Nzoia ameelezea umuhimu wa matumizi ya Neti ya kuzuia mbu na msambao wa ugonjwa wa malaria, akiongeza kuwa Neti hizo zitatumika kwa zaidi ya miaka mitatu.
By Imelda Lihavi