Chama cha UDA kinacho husishwa naye Naibu Rais dakta William Ruto kimezindua zoezi la kuwasajili wanachama katika eneo bunge la Likuyani katika juhudi za kukipa umaarufu na uungwaji mkono mashinani mbele ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Akizungumza alipozindua zoezi hilo kwenye hafla iliyooandaliwa katika eneo la Soy, kaimu mwenyekiti wa chama hicho tawi la Likuyani Deberious Shikuku Wafula amefichua kuwa tayari chama hicho kimewa vutia zaidi ya wafuasi elfu 15 eneo hilo , akihoji kuweka mikakati ya kuuza sera za chama hicho mashinani na kuhakikisha kinashinda viti vingi mno kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Aidha Deberious amepuuziliambali madai kuwa eneo la magharibi ni ngome ya vyama vya ANC na Ford Kenya.
By Richard Milimu